Akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari Mkurugenzi mtendaji wa CEO ROUNDTABLE TANZANIA Ndugu Santina Benson, CEOrt inaongozwa na kanuni za uongozi wa kimaadili na inakuza ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi nchini Tanzania, ikidhamiria kuongeza kasi ya kupanua na kukuza uchumi wa Tanzania. Maeneo ya kipaumbele katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Tanzania 2021/22-2025/26 ni pamoja na kuchochea uchumi shindani na kukuza uwekezaji na biashara. Katika hotuba yake ya Mwisho wa Mwaka 2021, Rais Samia aliuita mwaka 2022 kuwa ni mwaka wa ukuaji wa uchumi, na kusisitiza kuwa katika mwaka huu lengo kuu la utawala wake ni kukuza uchumi na ustawi wa Watanzania, kama ilivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa.
Kupitia nguzo yake ya Maadili, CEOrt ilifanya kazi kwa kushirikiana na sekretarieti ya maadili kuandaa Ahadi ya Kitaifa ya uadilifu kwa viongozi wa umma, watumishi wa umma na sekta binafsi. Ahadi hii inaonyesha kujitolea kwa mtu kudumisha tabia ya kimaadili na kanuni za kupinga ufisadi, na wanachama wa CEOrt wanaongoza kwa mfano ikiwa 99% wakiwa tayari wametia saini ahadi hiyo. Katika nguzo yake ya Ushirikishwaji, CEOrt huandaa mashirikiano kati ya wanachama, serikali na washirika wa maendeleo, na kuwezesha ubia wa sekta binafsi kwa maendeleo endelevu, ambayo hufungua njia kwa mijadala juu ya sera na juhudi za utetezi shirikishi kwa ajili ya kuboresha biashara na mazingira ya uwekezaji.
Shirika linawakilisha Wakurugenzi Wakuu kutoka kampuni zaidi ya 150 zinazoongoza nchini Tanzania kutoka sekta mbalimbali za uchumi kwa madhumuni ya pamoja ya kuongeza matokeo katika uongozi na ustawi endelevu wa jamii na uchumi wa nchi. Kwa pamoja, wanachama wa CEOrt huchangia katika uchumi wa Tanzania kupitia ukusanyaji wa kodi, ajira, kujenga uwezo, kuhamisha teknolojia na kuongeza ujuzi.
Baadhi ya wadau wakifuatilia mkutano wa CEO ROUNDTABLE Ulio fanyika Tarehe 8, Februari 2022, katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam