Msanii maarufu kutoka Kenya, KRG The Don, ameweka wazi nia yake ya kuwania kiti cha Ubunge katika Jimbo la Naivasha mwaka wa 2027. Akiwa mgeni katika kipindi maarufu cha Hitzone ndani ya Jembe fm kinachoendeshwa na watangazaji Nattyebrandy na B 45, KRG alifunguka kuhusu mipango yake ya kisiasa na dhamira yake ya kuwatumikia wananchi wa Naivasha.
Katika mahojiano hayo, KRG The Don alisema:
“Watu wa kwetu wananikubali na kazi zangu na wamesema wako tayari nikiwasaidia kutatua changamoto zao, hivyo najipanga.”
Ameeleza kuwa mapenzi na uungwaji mkono anaopata kutoka kwa watu wa Naivasha ndio yamempa moyo wa kuchukua hatua hiyo kubwa. Alisisitiza kuwa muda umefika kwa vijana na watu wenye ushawishi kuingia kwenye uongozi ili kuleta mabadiliko ya kweli.
KRG, ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kupitia muziki wake na uwepo wake kwenye mitandao ya kijamii, anaonekana kuwa na maono mapana ya kusaidia jamii yake.
Mpango huu wa kisiasa ni hatua mpya kwa msanii huyo ambaye tayari ana mashabiki wengi nchini na nje ya mipaka ya Kenya. Kama atatekeleza alichokisema, basi 2027 huenda ikawa mwaka wa kihistoria kwa Naivasha, huku burudani na siasa zikikutana kwenye jukwaa la maendeleo.
Kwa sasa, mashabiki wake na wakaazi wa Naivasha wanasubiri kuona kama KRG The Don atadumisha nia hiyo hadi sanduku la kura litakapowekwa mbele yao.wakati huo huo akiwa anafanya vizuri na kibao chake cha sina noma akiwa ameshirikiana na Arrow bwoy.