Mshambuliaji Mpya wa Man United bado kidogo tu

BADO ni suala la muda tu kabla ya Matheus Cunha kuwa mchezaji mpya wa Manchester United.

Nyota huyo wa Wolves amekubali kujiunga na United na tayari ametoa mwanga wa kijani kwa uhamisho huo kukamilika.

Makubaliano binafsi yameshakamilika, na sasa klabu hiyo ya Old Trafford imeanza mazungumzo ya mwisho na Wolves kuhusu malipo ya pauni milioni 62.5 kwa awamu.

Hakuna pingamizi kubwa linalotarajiwa katika hatua hii, huku vipengele vya mwisho vya mkataba vikikamilishwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii