Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amesema serikali haiwezi kuingilia mgogoro unaoendelea kuhusu mechi ya Darby kati ya Simba na Yanga kutokana na kuwepo mamlaka inayosimamia soka nchini ambayo ni TFF.
Mwinjuma amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Jimbo la makete Festo Sanga aliyetaka kujua hatima ya mvutano wa timu mbili za Simba na Yanga pamoja na TFF
Aidha ameeleza kuwa Shughuli za mpira wa mguu unamamlaka zake za kimataifa na za kitaifa na wamekuwa wakisisitizwa mara kwa mara serikali kutoingilia moja kwa moja kutoingiloa uendeshaji wa shughuli hizo ili kuepuka kuja kufungiwa na FIFA kwa nyakati hizi hata kitakwimu nchi yetu inafanya vizuri katika uendeshaji wa shughuli za mpira wa miguu.
Hata hivyo ameongeza kuwa katika mchezo anaousema serikali inafuatilia kwa karibu jinsi ambavyo mgogoro huu unaendelea kutatuliwa lakini huku tukijaribu kwa kiwango kikubwa kutoingilia moja kwa moja maamuzi ya TFF na Bodi ya ligi.