Serikali iiko kwenye mpango madhubuti wa kukarabati uwanja wa CCM Kirumba

Serikali imesema bado iko kwenye mpango madhubuti wa kuhakikisha uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza unakarabatiwa na kukamilisha idadi ya viwanja vitano vilivyotengwa kwa ajili ya kusaidia viwanja vitakavyotumika katika Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma wakati akijibu swali la Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula ambapo alihoji ni lini serikali itaanza kukarabati uwanja huo kwa ajili ya matumizi ya michuano ya AFCON.

Hata hivyo Mwinjuma amesema kuwa viwanja hivyo vitano ambavyo serikali imevitaja havitatumika moja kwa moja kwenye mashindano hayo wakati viwanja vitakavyotumika ni  Benjamini Mkapa, Dar es Salaam, Uwanja wa Arusha na New Amaani Complex Zanzibar.

Aidha Sasa hivi nguvu kubwa ya serikali imewekwa katika viwanja vitakavyotumika kwenye michuano ya CHAN na AFCON hivyo kituo cha mafunzo cha Ilemela kitaanza baada ya viwanaja hivyo kukamilika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii