Maamuzi mabovu ya waamuzi ligi kuu Tanzania, Mwigulu aahidi kuleta VAR

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema atakaa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa ili waongee uwezekano wa kutenga bajeti ya kununua VAR na nyasi bandia.

Mwigulu ameeleza hayo kupitia Ukurasa wake wa Instagram akitolea mfano wa nafasi aliyonyimwa mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele kufunga goli dhidi ya Mbeya City mwamuzi akidai ameotea.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii