Uwanja wa Mkapa upo tayari, wenye maamuzi ni CAF

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji mkuu wa Serikali ametembelea na kukagua maendeleo ya ukarabati wa uwanja wa Benjamin william Mkapa na kulidhishwa na hatua ya marekebisho na Ukarabati wa miundombinu, Ufungwaji wa viti vipya, Uboreshaji wa vyumba vya wachezaji, Unoreshaji wa vyumba vya waamuzi na na uboreshaji wa eneo la kuchezea ( Pitch) na mpaka sasa ukarabati umefikia asilimia 85 na ubora wa uondoaji maji ndani ya uwanja ( Pitch) umeongezeka mara kumi zaidi ya kabla.


Aidha pia serikali kutoa Zaidi ya billion 650 kwa ujuenzi wa viwanja vipya viwili ikiwemo kiwanja cha Dodoma na Arusha na hatua ya ujenzi wa uwanja wa Arusha umefikia asilimia 43 na pia uwanja wa Uhuru utaboreshwa kufikia kiwango Cha Kimataifa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii