SIMBA WATWAA MEDALI BINGWA WATETEZI KOMBE LA SHIRIKISHO

Klabu ya Simba SC ya Tanzania
imefanikiwa kushika nafasi ya pili katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) msimu wa 2024/25, baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya RS Berkane ya Morocco katika mchezo wa marudiano wa fainali uliopigwa katika viwanja vya New Amani Zanzibar.

Kwa matokeo hayo RS Berkane wamefanikiwa  kutwaa ubingwa kwa jumla ya mabao 3 dhidi ya Simba SC huku simba ikishika nafasi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika 2024/25.

Kutokana na  matokeo hayo RS Berkane wametwaa ubingwa kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa mabao 2-0 nyumbani kwao Morocco.

Mchezo wa jana uliokuwa wa kuvutia uliojaa ushindani mkubwa ambapo Simba SC walionyesha moyo wa kupambana mbele ya mashabiki wao lakini hawakuweza kufuta tofauti ya mabao matatu yaliyopatikana katika mchezo wa awali huko nchini Morocco.

Hivyo Simba Sc club wamefanikiwa kuwa mabinga watetezi wa kombe la shirikisho barani Afrika na kuvaa medali jambo ambalo limeweka rekodi kwa timu nzima pamoja na uongozi vile vile katika upande wa Rs berkane ya nchini Morocco  mabimgwa waliotwaa kombe wakiwa katika nafasi ya kwanza.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii