Kuelekea fainali ya UEFA Europa League hapo kesho Jumatano Mei 21 kwenye Uwanja wa San Mames Marria, Bilbao, Spain, majira ya Saa Nne kamili usiku, klabu ya Man United imeamua kufunga busta kwa kuwaongeza kikosini wachezaji wake Leny Yoro, Diogo Dalot na Joshua Zirkzee, ambapo hii leo wamefanya mazoezi ya pamoja na timu huko Carrington.
Wachezaji hao walikuwa na changamoto ya majeraha na kulikuwa na hofu ya kukosekana kwao katika mchezo huo. Man United wameingia katika hatua hii ya fainali kwa kuwatoa Athletic Club Spain huku Spurs wakiwaondosha Bodo/Glimt ya Norway.