Bunge la Iraq limepitisha sheria ya kuruhusu watoto wa umri wa miaka tisa kuolewa, huku wanaharakati wakisema kuwa hatua hiyo itahalalisha ubakaji wa watoto.
Sheria hiyo imebainisha kuwa Waislamu wa Shia ambao ndio wengi zaidi nchini Iraq, umri wa chini zaidi wa kuolewa utakuwa miaka tisa, na wa Sunni, umri rasmi utakuwa miaka 15.
Sheria hiyo mpya inazipa mahakama za Kiislamu, mamlaka zaidi katika kushughulikia masuala ya kifamilia kama vile ndoa, talaka, na mirathi, huku ikiondoa sheria ya hapo awali inayokataza ndoa za watoto walio chini ya umri wa miaka 18, ambayo imekuwepo tangu miaka ya 1950.