KEVIN POWELL AMSHUTUMU SNOOP DOGG KUWA MSALITI

Kufuatia kuapishwa rasmi kwa Donald Trump kuwa raisi wa Marekani kwa mara nyingine tena baada ya ushindi wake katika uchaguzi uliopita dhidi ya mpinzani wake Kamala Harris 

Kwa sasa kumeibuka mijadala juu ya wanamuziki walioshiriki katika sherehe za uapisho wake , kabla na siku ya uapisho wake wapo wasanii ambao walipata nafasi ya kutumbuiza miongoni mwao ni rapa maarufu Snoop Dogg

Mwandishi wa habari na mtangazaji Kevin Powell amemtupia lawama rapa huyo Snoop Dogg kwa kutumbuiza  kwenye sherehe za awali kwenye uapisho wa Donald Trump na kukuiita kitendo iko kuwa ni Usaliti 

Kevin anasema kwamba kitendo hiko ni Usaliti kwa mashabiki na jamii nzima inayomzunguka Snoop Dogg, Kupitia mahojiano hayo na TMZ Kevin Powell anasema kuwa ...

Snoop Dogg hakuwa hivo mwanzo na anatolea Mfano zamani namna ambavyo Snoop alikuwa mstari wa mbele kutetea jamii yake na kwa sasa ni kama amewasaliti na kufuata pesa

Sio tu kwa Snoop Dogg, Kevin Powell pia amemkosoa nyota wa Muziki wa country  Carrie Underwood ambae anafahamika kwa utetezi wa mapenzi ya jinsia moja pamoja na sela ya udhibiti kwenye matumizi ya silaha ambae pia ali tumbuiza kwenye sherehe hizo za uapisho wa  Donald Trump ambae ni wazi anapinga mahusiano ya jinsia moja Kwa kutambua uwepo wa jinsia mbili pekee Me na Ke

Kwa ujumla Kevin amewakosoa wasanii wote ambao walishiriki kwenye hizo haswa wasanii wa Muziki wa Hip-Hop ambao asili ya Muziki wanao ufanya unatoka kwenye jamii ya watu wa chini watu maskini ambao wanawaitaji wasanii kuwasemea hivyo kitendo cha wasanii hao kushiriki kwenye sherehe hizo kwake ni kama usaliti.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii