RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Dk. Patrice Motsepe, amechaguliwa tena kuliongoza Shirikisho hilo kama Rais kwa kipindi cha miaka minne ijayo.
Motsepe ambaye amekuwa Rais wa Shirikisho hilo tangu mwaka 2021, sasa atasalia katika kiti hicho mpaka mwaka 2029 Kwa awamu ya pili mfululizo.
Uchaguzi huo umefanyika leo Machi 12,2025 jijini Cairo Nchini Misri katika Mkutano mkuu Usio wa Kawaida wa 14 wa CAF.
Rais wa Fifa, Gian Infantino, Rais wa TFF na CECAFA Wallece Karia, Rais wa Yanga Sc na mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu Africa, Eng. Hersi Said pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba Sc Salim Abdallah “Try Again” ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria uchaguzi huo.