TFF Yavifungia Viwanja Vitatu Vya Ligi Kuu Kwa Kutokidhi Vigezo

hirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limevifungia viwanja vya Jamhuri (Dodoma), CCM Kirumba (Mwanza), na Liti (Singida) kutumika kwa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na kushindwa kufikia vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

Uamuzi huu umechukuliwa baada ya tathmini kubaini mapungufu mbalimbali katika viwanja hivyo, ikiwemo hali ya nyasi, miundombinu ya wachezaji na mashabiki, pamoja na usalama kwa ujumla. Hatua hii inalenga kuboresha mazingira ya mchezo na kuhakikisha viwanja vinakidhi viwango vinavyotakiwa kwa soka la ushindani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii