Watafiti hao wenye makao yao mjini Washington pia wanasema mazoezi hayo ya Iran yalianza mwishoni mwa Disemba, na yalitarajiwa kukamilika katikati ya mwezi Machi, yakihusisha baadhi ya mifumo ya silaha ambazo ni tishio kwa Marekani na Israel huku mengine yakifichua udhaifu katika uwezo wa Iran wa kujilinda.
"Kasi, nguvu na utangazaji wa mazoezi hayo hayajawahi kutokea," Behnam Ben Taleblu wa Wakfu wa Ulinzi wa Demokrasia amesema. Farzin Nadimi kutoka Taasisi ya Washington ya Sera za Mashariki amesema amekuwa akisomea masuala ya kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu kwa muda wa miaka 20 iliyopita."Sijawahi kuwaona wakifanya mazoezi mengi kwa muda mfupi hivyo kama ilivyo shuhudiwa," alisema.