Mvutano kati ya MarthaMwaipaja na mdogo wake BeatriceMwaipaja umechukua sura mpya baada ya sauti zao wakishambuliana kwa maneno makali kusambaa mitandaoni. Katika sauti hizo, wawili hao wanasikika wakitupiana lawama kali, huku Beatrice akimtuhumu dada yake kuwa ameikataa familia yake.