Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria ambaye amefanikiwa kuwa kwenye muziki na kiwanda cha Sanaa kwa miaka kadhaa Nasboi ambaye amefanikiwa kufanya kazi nyingi na wasanii mbali mbali nguli kutoka nchini Nigeria akiwemo olamide.
Ameachia wimbo wake mpya akiwa ameshirikiana na mkali wa muda mrefu kutoka nchini humo D’ banj wimbo ambao umepewa jina la Compose.
Wimbo huu umekutanisha wabunifu wawili wenye karama ya aina yake katika muziki na Sanaa kwa ujumla ambapo ukisikiliza si kwamba utafurahia peke yake bali utaendelea kufurahia ubunifu wao binafsi.
Ni wimbo ambao unapatikana katika vyanzo mbali mbali vya kupakua muziki kwa ujumla.