Rais Dkt. Samia Ashiriki Hafla Ya Utoaji Tuzo Za Wasanii Wa Komedi, Washindi

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Jumamosi Februari 22, 2025 amesema Serikali itaendelea kuwashika mkono wasanii wa ucheshi ili wafike ngazi za kimataifa na kunufaika na vipaji vyao.

Rais Samia ameyasema hayo katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha tuzo hizo ambazo zimehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo mawaziri, wasanii na wakuu wa taasisi za umma na binafsi.


Rais Samia amesema wazo lililotolewa na wachekeshaji la kucheza mchezo wa ‘upatu’ linaweza kuwa zuri endapo likibadilishwa na kutafutiwa namna bora ili kusaidia masuala ya kifedha ya nchi za Kiafrika.

Rais Samia amesema wazo hilo likichukuliwa kitofauti litakuwa na mchango wa kujitegemea kifedha, kama wakikubaliana na viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuunda mfuko wao.

Wafuatao ndio walioibuka kidedea Tanzania Comedy Award 2024/2025;

Champion Of Comedy – Rais Samia Suluhu Hassan
Hall Of Fame – King Majuto (Legendary!)
Tuzo ya Heshima – Ccoy Mzungu
Best Comedian Actor Of The Year – Joti
Best Comedy Special Award – Juma Omary Laurent (Jolmaster)
Best Male Comedian Of The Year –Nanga
People’s Choice: Best Comedian Of The Year – Laughs On Leonardo
Best Female Comedian Of The Year – Asmah Majed
Best Male Stand-Up Comedian – Eliud Samwel

Best Female Stand-Up Comedian –Neyla Manga

Best Funny Leader Of The Year – Makongoro Nyerere
Legend People’s Choice – Joti
Best Comedy TV Show – Kitimtim

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii