Rapa na Emcee kutoka Uingereza mwenye asili ya Zimbabwe Rhyme Assassin ameachia rasmi video ya wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Run Em Up ( Told Ya )
Wimbo huu unatoka kama wimbo wa pili wa utangulizi katika album yake mpya Rhyme Assassin inayotarajiwa kutoka mwaka huu 2025
Kupitia wimbo huo wa kushirikiana Rhyme Assassin amemshirikisha M.O.P na James Brown kutoka Ruste Juxx, huku kwenye upande wa video ya wimbo huo imeongozwa na Entity Production
Rhyme Assassin ni miongoni mwa ma Emcee wenye uwezo wa kurap kwenye beat mbalimbali. Neno Rhyme kwenye jina lake ni kielelezo cha ushairi wake lakini neno Assassin kisanaa linaashiria uwezo wake ambao ni kipaji cha juu sambamba na ubunifu.