Kijiji cha Italia chawaamuru wakazi wasiugue

Kijiji cha Belcastro, kilichopo kaskazini mwa Calabria, Italia, kimewaamuru wakazi wake kuepuka magonjwa makubwa yanayohitaji huduma za dharura.

Belcastro ni miongoni mwa maeneo maskini zaidi nchini Italia, na Meya Antonio Torchia alisema kuwa amri hiyo ni “dhihaka ya mzaha,” lakini inaleta umakini kwa matatizo ya mfumo wa afya katika eneo hilo.

Takriban nusu ya wakazi 1,200 wa Belcastro wana zaidi ya miaka 65, na idara ya Dharura na Ajali (A&E) iliyo karibu iko zaidi ya kilomita 45 (maili 28) kutoka kijijini, alisema meya

Akionekana kufafanua kilichomchochea kutangaza amri hiyo alisema kuwa idara ya Dharura na Ajali inapatikana tu kwa usafiri wa barabarani ambao kikomo chake ni ,wendo wa kilomita 30 kwa saa.

Zahanati ya daktari wa kijiji hufunguliwa kwa vipindi vya mara kwa mara tu na haina huduma za dharura wakati wa wikendi, likizo, au baada ya saa za kazi.

Torchia aliiambia televisheni ya Italia kuwa ilikuwa vigumu “kujisikia salama unapojua kuwa ukihitaji msaada, tumaini lako pekee ni kufika kwenye kituo cha dharura kwa wakati” – na kwamba barabara ni “hatari zaidi kuliko ugonjwa wowote.”

Katika tangazo hilo, wakazi pia wameamriwa “kutofanya vitendo vitakavyoweza kuleta madhara na kuepuka ajali za nyumbani,” na “kutoshinda nyumbani mara kwa mara, kusafiri au kufanya michezo. Badala yake wameshauriwa kupumzika kwa muda mwingi.”

Haijulikani jinsi sheria hizi mpya zitavyotekelezwa vipi.

Calabria ni moja ya maeneo mfumo wake wa afya umeathiriwa na uongozi mbaya na uingiliaji wa makundi ya kihalifu.

Serikali kuu imekuwa ikisaidia kuondoa madeni ya hospitali, lakini wakazi wengi hulazimika kutafuta huduma za afya nje ya kanda.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii