Waombolezaji ambao walijumuisha maafisa kadhaa waliochaguliwa pamoja na makamu wa rais Kamala Harris, waliangazia baadhi ya mafanikio yake na ubinadamu wa kiongozi huyo aliyefariki mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 100.
David Smith profesa kwenye chuo cha Carter cha Amani na Usuluhishi wa Mizozo kwenye chuo kikuu cha George Mason, alisema kuwa rais huyo wa zamani alikuwa na ushawishi mkubwa kwenye maisha yake.