Manchester City yarejesha matumaini mapya kwa mashabiki

Ushindi wa mabao 3-0 walioupata Manchester City dhidi ya Leicester City umerejesha matumaini ya kikosi cha Pep Guardiola kilichoanzafa vibaya kwa msimu huu. Ushindi huo ni wa 9 katika mechi 19 walizocheza msimu huu wakipoteza mechi 6 na sare 4 wakijikusanyia alama 31 pekee.

Manchester City imetofautiana na Liverpool wanaoongoza ligi kwa alama 14. Swali ni je Manchester City itafanya maajabu wakati wa raundi ya pili ya EPL na kutetea ubingwa wake walioshinda msimu wa 2023/24?

Tathmini ya Mchezo wa Manchester City dhidi ya Leicester City

Pep Guardiola alifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 baada ya kuanza na Ortega golini akilindwa na Lewis ,Akanji,Ake na Gvadiol. Eneo la kiungo liliundwa na Kovavic,Foden,Benardo Silva,De Bruyne na Savio na safu ya ushambuliaji iliongozwa na Erling Halaand akitumia mfumo wa 4-1-4-1.

Katika mchezo huo Savio walijipatia bao la kwanza dakika ya 21 na Erling Halaand alifunga bao la pili dakika ya 74 ya mchezo. Bao hilo limefunga mwaka 2024 kwa Manchester City na kuweka matumai mapya kuelekea mwaka 2025.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii