Vijana na wananchi mbalimbali nchini
wameshauriwa kwenda Makumbusho ya Azimio la Arusha kujifunza misingi
muhimu iliyowekwa na waasisi wa nchi hii wakiongozwa na Hayati Baba wa
Taifa Mwl Julia Nyerere 1967.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi
wa Makumbusho ya Azimio la Arusha Dkt Gwakisa Kamatula kwenye
Maadhimisho ya miaka 55 ya Azimio la Arusha yanayoendelea katika Viwanja
vya Makumbusho hiyo iliyopo Jijini Arusha.
Dkt Kamatula amesema
kuwa wameamua kuanzisha maadhimisho hayo ili kupanua wigo wa kutoa
elimu na kuirithisha jamii urithi adhimu wa Azimio la Arusha hasa kwa
kizazi cha sasa ambacho hakina uwelewa mpana kuhusu misingi imara ya
nchi iliyosimikwa kupitia Azimio hilo.
" Waasisi wa Taifa letu
chini ya Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere, baada ya Uhuru
walikutana Arusha na kuweka misingi imara iliyosaidia na inaendelea
kusaidia kusukuma maendeleo ya nchi misingi hiyo ni kama vile Umoja wa
Kitaifa, Uwajibikaji, Udugu na Umoja, Utu, Uchapaji kazi kwa faida ya
wote nk" Dkt Kamatula
Naye Mratibu masaidizi wa Maadhimisho hayo
Bi Elizabeth Solomoni amesema maadhimisho ya Mwaka huu yamehusisha Mada
na Maonesho ya Vitu halisia vilivyotumika katika Mkutano wa Azimio,
Majadiliano, wajasiriamali na burudani ya sanaa mbalimbali.
Wakazi
mbalimbali waliotembelea kwenye Maadhimisho hayo akiwepo Bw Juma Kombo
mkazi wa Babati wameipongeza Makumbusho ya Taifa kupitia kituo cha
Makumbusho ya Azimio la Arusha kwa hatua iliyoichukuwa ya kuanzisha
Tamasha la Azimio la Arusha kwani kupitia Tamasha hilo watu wengi
watakuwa na hufahamu mkubwa wa umuhimu wa kuishi katika misingi ya
Azimio hilo.
" Watoto wetu wengi hawana ufahamu kabisa juu ya
Misingi iliyowekwa katika Azimio hili, wamekuwa wakifuata misingi ya
nchi zingine, wengi wamejaa ubinafsi, wengine wanawauwa hadi wazazi wao
hawana Utu, heshma imepungua, lakini kwa njia hii hakika sisi wazazi
tunapata matumaini' Mzee Juma Kombo
Tamasha limeanza tarehe 1
Feb 2022. na litafungwa na kuzindua miradi ya ustawi wa taifa na
mapambano dhidi ya UVIKO 19 inayotekelezwa katika vituo vya Azimio la
Arusha na Elimu viumbe, Jijini Arusha