Kombora hilo limesababisha ving’ora kulia, lakini hakuna uharibifu umeripotiwa baada ya kuzuiliwa kabla ya kuingia Israel.
Waasi wa Houthi walio nchini Yemen wamekuwa wakifyetua makombora kuelekea Israel tangu wanamgambo wa Hamas waliposhambulia Israel Oktoba 7 2023, na kupeleeka vita kuanza katika ukanda wa Gaza.
Israel imekuwa ikijibu mashambulizi ya waasi wa kihouthi kwa kutumua makombora ya angani.
Waziri wa ulinzi Israel Katz, ameonya kwamba viongozi wa Houthi watakabiliwa vilivyo namna wa Hamas walivyokabiliwa, sawa na viongozi wa kundi la wanamgambo la Hezbollah nchini Lebanon ambao wameuawa katika mashambulizi ya Israel.
Wanamgambo wa Hamas, Hezbollah, na Houthi wanaungwa mkono na Iran na makundi hayo yanatambuliwa na Marekani kama makundi ya kigaidi.
Wakati huo huo, Katz amethibitisha kwamba Israel ndio ilihusika na shambulizi la mwezi Agosti mjini Tehran, Iran, lililomuua kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh