Ndege ya Shirika la Ndege la Azerbaijan iliyokuwa imebeba watu 67 imeanguka karibu na mji wa Aktau nchini Kazakhstan na kusababisha vifo vya watu 38 waliokuwa ndani, kwa mujibu wa Mamlaka za Kazakhstan.
Katika operesheni kubwa ya uokoaji, manusura 28 wakiwemo watoto wawili waliokolewa kutoka kwenye mabaki ya ndege hiyo, Naibu Waziri Mkuu wa Kazakhstan, Kanat Bozumbayev, alisema, na kuongeza kuwa 11 wako katika hali mbaya.
Ndege ya Azerbaijan Airlines, safari ya J2-8243, ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa Azerbaijan, Baku, kuelekea Grozny katika eneo la Chechnya nchini Urusi kabla ya kutua kwa dharura umbali wa takribani kilomita 3 (maili 1.8) kutoka Aktau, shirika hilo la ndege lilisema.
Picha za eneo la ajali zilionyesha wakati manusura waliokuwa wameduwaa walipojitokeza kutoka kwenye mabaki ya ndege iliyoteketea.
Uchunguzi wa awali unasema kwamba ndege ya shirika la ndege la Azerbaijan iliyoanguka na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 30, ilitokana na ndege hiyo kugonga nyuki.
Taarifa zinasema kwamba ndege hiyo ililazimika kubadilisha safari kuelekea Aktau kutokana na tukio la dharura kwa abiria.