Watu 32 wamefariki dunia, baada ya mgodi wa Kobalti kuporomoka katika eneo la uchimbaji madini la Kalando, katika machimbo ya Mulondo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Ajali hiyo ilitokea baada ya milio ya risasi inayodaiwa kuzuka kutoka kwa wafanyakazi wa usalama waliokuwa wakilinda eneo hilo, na kusababisha wachimbaji kutumbukia kwenye mgodi wa wazi.
Akizungumzia tukio hilo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Mkoa wa Lualaba, Roy Kaumba Mayonde, alisema, licha ya marufuku rasmi ya kuingia kwenye eneo hilo kutokana na mvua kubwa na hatari ya maporomoko ya ardhi, wachimbaji walilazimisha kuingia kwenye machimbo hayo.
Aliongeza kusema kuwa, kuvuka kwa haraka kwa wachimbaji kulisababisha kuanguka kwa daraja la muda ambalo walikuwa wamejenga ili kuvuka mtaro uliofurika.
Mamlaka zinasema hadi sasa miili 32, imepatikana huku shughuli za utafutaji na uokoaji zikiendelea.