Mashambulizi ya Israel yamewaua watu watatu

Lebanon kupitia wizara yake ya afya imesema mashambulizi ya Israel kusini na mashariki mwa nchi hiyo, yamewaua watu watatu, licha ya makubaliano yanayoendelea ya usitishaji mapigano.

Lebanon kupitia wizara yake ya afya imesema mashambulizi ya Israel kusini na mashariki mwa nchi hiyo, yamewaua watu watatu, licha ya makubaliano yanayoendelea ya usitishaji mapigano. Israel ilisema kuwa mashambulizi yake yaliwalenga wanachama wawili wa kundi la wanamgambo la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran.

Katika taarifa iliyotolewa Jumapili, jeshi la Israel lilisema limemuua Ali Hussein al-Mousawi mashariki mwa Lebanon, likimtaja kama muuzaji wa silaha na msafirishaji haramu wa Hezbollah.

Aidha jeshi hilo lilisema pia limemuua mwanachama mwingine wa Hezbollahaliyetambulika kama Abd Mahmoud al-Sayed, kusini mwa Lebanon.

Umoja wa Mataifa ulisema Jumapili kwamba ndege isiyo na rubani ya Israel iliangusha guruneti karibu na kikosi chake cha kulinda amani huko Kfar Kila, kusini mwa Lebanon na pia kikosi chake cha doria kilishambuliwa na Israel.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii