Mithika Linturi Amlima Ruto kwa Madai ya Kuwatenga Wameru katika Uteuzi Serikalini: "Tumechoka"

Meru - Aliyekuwa Waziri wa Kilimo Mithika Linturi ameikosoa serikali ya Rais William Ruto kwa madai ya kuwatenga jamii ya Ameru.

Linturi alidai kuwa jamii ya Ameru imetengwa kutoka kwa maamuzi muhimu ya kisiasa kitaifa licha ya kuunga mkono kwa wingi Muungano wa Kenya Kwanza katika Uchaguzi Mkuu wa 2022. Linturi alilalamika kuwa serikali ya Ruto imekuwa ikidharau jamii ya Ameru na kushindwa kutambua mchango wao katika ushindi wake wa uchaguzi. “Ni muhimu heshima ya watu wa Meru irudi; tumechoka kudharauliwa. Tumechoka kuangaliwa kwa macho kana kwamba sisi ni watu wasio na maana... kura zetu 800,000 lazima zihesabiwe! Tulikubali na kuamini; sasa kuna dharau nyingi,” Linturi alisema.

Seneta wa zamani wa Meru alitishia kuongoza jamii hiyo kumkataa Ruto kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Kwa mujibu wa Linturi, rais anafikiri kwamba kwa kupata uungwaji mkono wa kiongozi wa ODM Raila Odinga, tayari amejihakikishia ushindi katika uchaguzi ujao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii