Prof.
Kahyarara ameyasema hayo alipokutana na kuongea na wasambazaji wa
bidhaa za vifaa vya ujenzi Dodoma, Februari 3, 2022 kuhusu sababu za
upandishaji wa bei na kupokea maoni ya jinsi ya kukabiliana na suala
hilo ili kukuza biashara na kuwalinda walaji na kutimiza lengo la
Serikali katika kujenga uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya
taifa na wananchi.
Aidha, Katibu Mkuu huyo, aliwashauri
wafanyabiashara na wasambazaji hao kujiandaa na kufanya biashara kwa
ushindani pamoja na kuchangamkia fursa za Mkataba wa Kuanzisha Eneo Huru
la Biashara Afrika (AfCFTA) ambao Tanzania imeridhia na kujiunga.
Mkataba huo unalenga kuwezesha uwekezaji na ufanyaji biashara baina ya
nchi na nchi katika soko lenye watu takribani bilioni 1.3 linalotarajiwa
kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi, kibiashara na kijamii barani
Afrika
Nao, Wasambazaji wa bidhaa za ujenzi hususan saruji,
nondo na mabati jijini Dodoma, walipata fursa ya kutoa sababu
zinazochangia kupanda kwa bei ya bidhaa hizo ikiwa ni pamoja na kununua
bidhaa hizo kwa bei kubwa kutoka kwa wasambazaji wakubwa, gharama kubwa
za usafirishaji wa bidhaa hizo kutoka viwandani hadi maeneo yao husika
pamoja na kupanda kwa bei ya malighafi za kutengenezea mabati kutoka nje
ya nchi, bei kubwa ya kusafirisha malighafi hizo kutoka nje ya nchi.
Aidha,
wakitoa mapendekezo mbalimbali ya jinsi ya kukabiliana na upandaji wa
bei za vifaa vya ujenzi, Wasambazaji hao waliishauri Serikali kuanzisha
mfumo bei elekezi ya saruji kulingana na maeneo waliopo kijiografia
pamoja na kuwashauri wamiliki wa viwanda kuboresha mfumo wa usambazaji
wa bidhaa kwa kuruhusu kuwa na wasambazaji wa bidhaa zao wengi badala ya
kuwa na wasambazaji wakubwa wachache.
Akipokea maoni na
mapendekezo hayo, Prof. Kahyarara aliwapongeza wasambazaji hao kwa
maoni na mapendekezo yao muhimu na kuahidi kuyafanyia kazi huku
akiwashauri kipunguza bei za bidhaa za vifaa vya ujenzi kuwa katika hali
halisi bila kuwaumiza walaji wa mwisho ili kujenga uchumi imara.