Makocha wa Simba SC na KMC wameongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo utakaoziktanisha timu zao siku ya kesho Novemba 6 kwenye uwanja wa KMC Complex Mwenge Dar es salaam. Wakufunzi hao wamezungumzia kuhusiana na maandalizi ya timu zao kabla ya kukutana uwanjani kesho.
Makocha wa Simba SC na KMC wameongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo utakaoziktanisha timu zao siku ya kesho Novemba 6 kwenye uwanja wa KMC Complex Mwenge Dar es salaam. Wakufunzi hao wamezungumzia kuhusiana na maandalizi ya timu zao kabla ya kukutana uwanjani kesho.
Kocha wa Wekundu wa Msimbazi Fadlu Davids amekiri ugumu wa mchezo dhidi ya KMC, ila anaamini juu ya ubora wa Wachezaji wa kikosi chake inaweza kuwa sababu ya wao kuondoka na ushindi dhidi ya Mpinzani wao. Kiungo wa timu hiyo Awesu Ally Awesu amethibitisha kukamilika kwa maandalizi upande wa wachezaji.
"Mchezo dhidi ya KMC haujawahi kuwa mchezo mwepesi, uwanja wa Manispaa ya Kinondoni unatumiwa na timu zote mbili kuwa wao wa nyumbani tunaamini tuna kikosi bora cha kupambana na kuondoka na matokeo ya ushindi dhidi yao"
"Maandalizi yetu wachezaji yamekamilika kwa sasa tunasubiri muda wa mchezo uweze kufika ili tutimize tuliyoyafanyia kazi mazoezini"
Kwa upande wa Kocha wa KMC, Abdihamid Moalin amesema kuwa anaheshimu kikosi cha Wapinzani wao siku ya kesho, ila amejipanga kuhakikisha KMC inafanya vizuri, Huku Mchezaji wa timu hiyo ya Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni Ibrahim Elias amewataka Mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi uwanjani.
"Naheshimu Simba SC kwakuwa ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri, Kocha Fadlu hajawahi kucheza dhidi yetu hii ni mechi yake ya kwanza , tumejipanga kufanya vizuri"
"Wachezaji tupo tayari kuwapa furaha Mashabiki, ikitokea tumepoteza ni bahati mbaya sio mapenzi yetu, niwaombe mashabiki wetu waje uwanjani kutupatia sapoti"
Simba SC itacheza dhidi ya KMC Jumatano Novemba 6,2024 katika uwanja wa Kmc Mwenge, Dar es salaam. Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kinashika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzani bara kikiwa kimejikusanyia alama 22 katika michezo 9 huku KMC ikiwa nafasi ya 6 imekusanya alama 14 katika michezo 10.