Wabunge wa Pakistan waongeza muda wa kuhudumu jeshini

Wabunge wa muungano unaotawala nchini Pakistan, waliidhinisha msururu wa miswada Jumatatu inayoongeza muda wa wakuu wa vikosi vya usalama, ikiwa ni pamoja na jeshi, kutoka miaka mitatu hadi mitano, licha ya maandamano ya upinzani.

Hatua hiyo ya kisheria inahakikisha kwamba Mkuu wa Jeshi Jenerali Asim Munir, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka miwili, ataendelea kuongoza jeshi lenye nguvu la nchi hiyo mpaka Novemba 2027.

Shughuli za bunge, zilizorushwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari, zilishuhudia maandamano ya kutatiza kutoka kwa wabunge wa chama cha upinzani cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI), kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani aliyefungwa Imran Khan, huku baadhi yao wakichana nakala za muswada na kuzirusha kwa spika wa bunge.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii