Cardi B " Hakuna MTU Ninaemchukia kama Offset"

Cardi B na Offset wamekuwa wakitengana na kurudiana mara kadhaa, lakini inaonekana uhusiano wao umeshindikana kabisa baada ya rapa huyo wa "Bodak Yellow" kumkandia tena Baba wa watoto wake watatu kwenye mtandao wa X akielezea namna anavyomchukia.


"Namtakia mabaya huyu mwanaume. Sijawahi kumchukia mtu kiasi hiki, na hawa wanawake walikuwa na kiu sana ya kuwa naye,Tafadhali mtu amchukue huyu mwanaume kutoka mikononi mwangu. Mfuko huu wa taka ni mzito sana!" Cardi B aliandika kwenye mtandao wa X Usiku wa Jumanne, Oktoba 22.


Mashabiki walijaribu kumtuliza, mmoja akisema, "Yeye ni baba wa watoto wako. Acha." Cardi alijibu kwa kusema, "Ndio, ni baba yao. Ndiyo maana sitamwombea afe, lakini namchukia sana … Familia yake na marafiki zake hawamwambii chochote. Ndiyo maana ataendelea kuwa mtu mbaya milele."


Hatahivyo Offset hajajibu lolote kuhusu kauli za Cardi. Mapema mwezi huu Offset pia alimshtumu Cardi kwa kuchepuka wakati akiwa mjamzito.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii