Kocha wa Liverpool Arne Slot ameweka wazi kuwa wanayo nafasi ya kushinda ubingwa wa mkombe yote ambayo timu yake inashiriki msimu huu wa 2024-2025. Slot ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa Waandishi wa habari kuzungumzia mchezo wa EPL utakaochezwa Novembe 2 Anfield.
Ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa Waandishi wa habari kuzungumzia mchezo wa ligi ambao utazikutanisha Liverpool FC dhidi ya Brighton and Hove Albion kwenye uwanja wa Anfield siku ya Jumamosi Novemba 2, 2024.
Liverpool FC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza nyuma ya Manchester City yenye alama 23 baada ya kucheza michezo 9 kila mmoja. Mchezo dhidi ya Brighton umatarajiwa kuwa mgumu kutokana na timu hizo zilicheza kwenye michuano ya kombe la Carabao katikati ya wiki na kikosi cha Majogoo ya Jiji ya Anfield kilipata ushindi wa goli 3-2, goli ambazo zilifunngwa na Cody Gakpo mbili na moja likifungwa Luis Diaz.
Brighton inashika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza ikiwa na alama 16 baada ya kucheza michezo 9, Seagulls inanolewa na Kocha raia wa Ujerumani anayeitwa Fabian Hürzeler baada ya Mkunzi wake raia wa Italia Roberto De Zerbi kutimkia kikosi cha Olympique de Marseille cha nchi Ufaransa.
The Reds bado imo kwenye makombe yote inayoshiriki msimu huu wa 2024-2025, Ligi kuu Uingereza, Ligi ya mabingwa barani Ulaya, kombe la Carabao na FA. Klabu hiyo yenye makao yake makuu Jijini Liverpool imewahi kushinda makombe matatu msimu mmoja miaka ya 1984,2001,2020. Slot anataka kuandika historia yake ndani ya Liverpool FC.
Liverpool imefuzu kucheza hatua ya robo fainali ya kombe la Carabao imejikusanyia alama 9 kwenye ligi ya mabingwa baada ya kushinda michezo yake mitatu na inashika nafasi ya pili EPL nyuma ya Manchester City ikiwa imejikusanyia alama 22.
Arne Slot amejiunga na Liverpool mwanzoni mwa msimu huu wa 2024-2025 mwezi Julai kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp. Anakazi kubwa ya kuwasahaulisha Mashabiki wa Majogoo ya Jiji mafanikio waliyoyapata kipindi cha Klopp kwa kushinda makombe walau mawili msimu huu.