Q NICHOLS NA YOUNG THUG WAKIRI KOSA MAHAKAMANI

Q Nichols mwenye umri wa miaka 29 ambae pia ni miongoni mwa watuhumiwa kwenye kesi ya YSL RICO inayomuhusisha rapa kutoka Nchini Marekani Young Thug na washirika wake amefanya makubaliano mahakamani na kukiri makosa yake.

Nichols alikutwa na hatia kwenye makosa yake lakini kulingana na makubaliano ambayo ame saini mahakamani amekutwa na hatia kwenye kosa moja na hivo ameondolewa makosa 6 ikiwemo kosa la mauaji sambamba na umiliki wa silaha kinyume na sheria.

Kupitia makubaliano hayo  judge Paige Reese amemuhukumu Nichols kifungo cha miaka 20 ambapo atatumimia miaka 7 akiwa jela lakini miaka 13 ataitumikia akiwa uraiani ambapo ni chini ya uangalizi kulingana na masharti aliyopewa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii