Mtayarishaji wa Muziki kutoka Nchini Marekani Metro Booming ameshitakiwa na Mwanamke mmoja ambae amefahamika kwa jina la Vannessa LeMaistre ambae anadai Metro Booming alimbaka na kumpa ujauzito wakiwa studio kwake mwaka 2016 huko Los Angeles.
Kwa mujibu wa TMZ Mwanamke huyo alifungua mashtaka hayo tarehe 29 ambapo kwenye maelezo yake anasema kwamba..
Metro Booming alimualika studio kwake mwaka 2016 ambapo akiwa studio alitumia vidonge sambamba na kunywa pombe kwa ajili ya kuondokana na msongo wa mawazo ambao ulitokana na kifo cha mtoto wake.
Baada ya kutumia pombe alisinzia lakini wakati anarejea kwenye ufahamu wake alishituka kukuta Metro Booming akiwa juu yake na alikua akifanya ngono kwa kutumia mdomo kwa kumnyonya sehemu zake za siri.
Baada ya kuona hivo anadai alizima tena na baada ya kuamka alijikuta yupo katika chumba cha Hotel moja huko Beverly Hills na Metro Booming akamwambia ni muda wa kuondoka na hakumbuki alifikaje hapo hotelini.
Kesi hii kwa Metro Booming inakuja wakati huu ambao anafanya vizuri kupitia kazi zake za Muziki ambapo anatajwa kama miongoni mwa watayarishaji bora wa Muziki kwa sasa.