Miss Rwanda Kupandishwa Mahalamani Baada ya Kuendesha Gari Akiwa Chakali Bila Leseni

Mshindi wa taji la urembo la Miss Rwanda mwaka 2022, Divine Nshuti Muheto anatarajiwa kufikishwa Mahakamani leo October 31,2024 baada ya Polisi Rwanda kuthibitisha kumkamata kwa makosa ya kuendesha gari akiwa amelewa na bila ya kuwa na leseni na kusababisha ajali iliyopelekea kuharibu miundombinu na kisha kukimbia eneo la tukio baada ya ajali.


Taarifa iliyotolewa na Polisi imesema hiyo sio mara ya kwanza kwa Mrembo huyo kutenda kosa la barabarani.

Mrembo huyo alipata umaarufu aliposhinda shindano la Miss Rwanda mwaka 2022, kabla ya Serikali ya Nchi hiyo kusitisha shindano hilo baada ya tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya Waandaji.

Adhabu ya kuendesha gari ukiwa umelewa Nchini Rwanda ni faini ya faranga 150,000 za Rwanda (Tsh. 299,200) na kuwekwa rumande kwa muda wa siku tano. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii