WIZARA YA AFYA YAPOKEA VIFAA TIBA KUTOKA PHARM ACCESS FOUNDATION

Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar imepokea msaada wa wa vifaa tiba ya mama na mtoto  vyenye thamani ya Tsh milioni 92 kwa lengo la kuimarisha afya bora nchini.

Akipokea msaada huo  huko Wizara ya Afya, Mnazimmoja Waziri wa Wizara hiyo Mhe, Nassor Ahmed Mazrui amesema  vifaa hivyo vitasaidia kupunguza tatizo la uhaba uliopo katika Hospitali za Unguja na Pemba.

Amesema ukosefu wa vifaa tiba ni jambo linalodhoretesha matibabu hasa kwa akina mama na mtoto hivyo kupatikana kwa vifaaa hivyo ni jambo jema ambalo litaweza kusaidia jamii.

Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa dawa, Waziri Mazrui amefahamisha kuwa kwa sasa dawa zilizopo hazitoshelezi kutokana na wingi wa wagonjwa  lakini  wanafanya jitihada zaidi kuhakikisha wananchi wanapatiwa matibabu ya uhakika

“Upatikanaji wa dawa hazitoshelezi kutokana na ongezeko la wagonjwa lakini tunajitahidi tuhakikishe  wananchi wetu wanapata dawa angalau kwa kiasi kilichopo,” alisema Waziri .

Hata hivyo  kwa Niaba ya Serikali Waziri huyo ameishukuru Taasisi ya PhamAcces Faundation kwa kuwapatia vifaa hivyo na kuwaomba kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuimarisha afya katika jamiii.

Nae Mkurugenzi wa PhamAcces Faundation Dkt Heri Marwa amesema kuwa lengo la kutoa msaada huo  ni kuimarisha afya ya mama na mtoto katika jamii.

Aidha amefahamisha kuwa wameamua kutoa msaada huo baada ya kufanya utafiti kwa kutumia data kupitia hospitali mbalimbali Unguja na Pemba na kugundua kuwa ipo haja ya kuongeza nguvu hasa kwa akina mama na watoto.

Msaada huo umejumuisha vifaa mbalimbali ikiwemo Delivery bed, BP machine digital,Digital thamometer, Heumaque machine,hospital Screen na Examination machine

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii