Rapa Card B amelazikika kusitisha show yake kwenye tamasha la Muziki ONE MUSIC FEST ikiwa ni muda mfupi kabla ya kuanza kwa tamasha hilo
Kupitia taarifa yake aliyoichapisha kwenye mtandao wa X Card B amesema kuwa amelazimika kusitisha show hiyo kutokana na changamoto za kiafya alizopata jambo ambalo limepelekea kulazwa
Card B ameamdika kuwa " Nasikitika kuwapa taarifa hii lakini nipo hospital kwa siku kadhaa sasa na naendelea vizuri , sitoweza kutumbuiza kwenye tamasha la ONE MUSIC FEST " Aliandika CARD B
" Nasikitika kwamba sitoweza kuonana na mashabiki zangu weekend hii na nilitamani sana kuwepo, Nashukuru kwa kunielewa nitarejea hivi karibuni nikiwa imara ,Nawapenda sana "
Card B alikua miongoni mwa watumbuizaji vinara kwenye tamasha hilo ambalo litafanyika October 26 & 27 huko Atlanta Central Park
Licha ya kutokuwepo kwa Card B , wasanii watakao tumbuiza kwenye tamasha hilo ni pamoja na Gunna,Sexyy Red,Nelly,Victoria Monet,GloRilla na wengine wengi