Maafisa katika mji wa Argentina wa Buenos Aires, wanajaribu kuzuwia mauzo ya mihadarati aina ya kokeni baada ya kuwauwa watu wapatao na wengine 70 kulazwa hospitalini baada ya kutumia dawa hiyo ya kulevya.
Maafisa wamewaonya wavutaji ambao hivi karibui walinunua kokeni kuacha kuitumia mara moja.
Akielezea kuhusu tukio hilo ,mwandishi wa habari aliyeko Buenos Aires -Frankie Deges, amesema: "Tetesi mbali mbali zinazunguka kuhusu ni nini hasa kilichotokea, ikisemekana kuwa kokeni hizo ilichanganywa na sumu ya kuua panya . "
Polisi tayari wamewakamata watu 10 wakiwashuku kuchanganya kokeni na madawa.