Baada ya YANGA kususia uwanja wa Azam Complex, na kutangaza kuhamia uwanja wa KMC Complex. CEO wa Azam, Abdulkarim Amin 'Popat' aliita kikao cha dharula kwa wafanyakazi wote wa uwanja wa chamazi na kufanya kikao kizito chenye lengo la kujua hasa nini chanzo cha mteja wao YANGA Kuondoka.
Kabla ya kikao hicho uchunguzi alioufanya POPAT Iligundulika kuwa zile video za kwenye CCTV ilikuwa ni mpango wa kutengeneza na wahusika wakuu ni wafanyakazi wa Uwanja wa Azam Complex akiwemo pia Meneja wa Uwanja huo.
Jamaa kawekwa kitimoto aeleze kitu ambacho kimetokea baada ya matukio ya CCTV Camera za uwanja huo kuvuja na kwanini vitendo vile vinatokea katika uwanja huo. Meneja alijitetea kuwa video zile hazikuwa serious na lilikua kama jambo la utani tu lakini mwisho wa siku limeleta taharuki kwa mabosi hao.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii