Ripoti ya Chombo Cha Habari.... ALL HIP-HOP kutoka Nchini Marekani imeibua document za mahakama zinazohusisha maombi ya kukataa rufaa kwenye hukumu ya kesi ya mauaji ya rapa Nipsey Hussle .
Ripoti hiyo imeeleza kuwa Erick Holder ambae alihukukiwa kwa kosa la mauaji ya rapa Nipsey Hussle alijaribu kutuma maombi yake kwa kutumia wanasheria wake akidai kukata rufaa kwenye kesi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo pia inaeleza ombi hilo lilikataliwa na sasa ataendelea kubakia jela na kutumikia kifungo chake cha miaka 60 baada ya kuhukumiwa mwaka 2023.
Kwenye kesi hiyo ya mauaji Erick Holder alikutwa na hatia kwenye makosa yake yote ikiwemo kosa la kufanya mauaji kwa kukusudia ambapo hukumu yake ilikua ni kifungo cha maisha na miaka 25 jela.
Makosa mengine mawili ya kufanya shambulio kwa mtu sambamba na kufyatulia risasi watu wawili.... kwenye makosa haya pia Erick alihukukiwa miaka 25 jela na miaka 10 mingine kwa kosa la kunyanyasa watu kwa kutumia silaha.