Mastaa mbalimbali wa Muziki duniani wamejitokeza kumpongeza Donald Trump ambae ameibuka mshindi dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake Kamala Harris kwenye kinyang'anyiro cha Uraisi Nchini Marekani
Baada ya ushindi huo wa Trump kutangazwa rasmi mastaa mbalimbali wameibuka na mitizamo yao ikiwemo pongezi kwenda kwa raisi huyo mpya wa Marekani
Miongoni mwa mastaa hao ni pamoja na 50 Cent ambae toka mwanzo alionesha kumuunga mkono Donald Trump licha ya kukataa ofa ya kutumbuiza kwenye moja kati ya mikutano ya kampeni zake
50 Cent kupitia ukurasa wake wa Instagram ameshare picha yake ya pamoja na Donald Trump ambapo aliambatanisha na ujumbe unao sema " Sijali mapambano yalikua vipi lakini naondoka na mshindi.... Bado sielewi ni nini kinaendelea. Hongera "
Kwa upande mwingine rapa Card B ambae yeye alikua akimuunga mkono mgombea wa Uraisi Kamala Harris ameandika ujumbe wake akionesha kutokuridhika na matokeo hayo huku akitupa lawama kwa watu wote waliopiga kura kwa Donald Trump na kuwaeleza kwamba ndio maana "Miji ama Majimbo yao huwa yanakumbwa na vimbunga " akimaanisha yawezekana watu hao wakawa na laana
Miji ambayo Card B anailenga hapa ni miji ama majimbo ya kusini Florida , Georgia & South Carolina
Mapema wiki hii Donald Trump alitangazwa kuwa mshindi kwenye kinyang'anyiro cha Uraisi Nchini Marekani baada ya kumshinda mpinzani wake Kamala Harris.