Rapa Young Thug amezungumza na wanafunzi wa chuo cha sheria Nchini Marekani na kuwahasa wanafunzi hao kuweka juhudi kwenye masomo yao ili kuja kusaidia watu mbalimbali wenye changamoto za kisheria kama ilivyokua kwake
Young Thug Amesema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa Sheria kutoka chuo Kikuu cha EMORY kupitia njia ya mtandao FaceTime ikiwa kama moja kati ya mafunzo kwa wanafunzi hao chini ya Mwalimu wao Brian Steel
Brian Steel ni Mwanasheria ambae alimsimamia rapa Young Thug kwenye kesi yake ya Ysl Rico na amewasisitiza wanafunzi hao kusoma ili waje kuwa watu muhimu kwenye jamii kama alivyo Brian Steel
Young Thug amefanya mazungumzo hayo ikiwa pia ni njia moja wapo ya kutekeleza masharti aliyopewa kwenye hukumu yake ya kifungo cha nje cha miaka 15 alichopewa kutokana na kesi iliyokua ikimkabili maarufu kwa jina la Ysl Rico.