KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga SC Stephane Aziz Ki ameamua kubeba jukumu zito la kuwapa furaha mashabiki katika dakika 90 za mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CBE.
Yanga inaondoka kesho kuelekea Zanzibar kwa ajili ya Mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya CBE ambao umepangwa kuchezwa Septemba 21, Uwanja wa New Amaan Complex.
-
Aziz Ki amesema dakika 90 za pili ni muhimu kwao kwa ajili ya mambo mawili, kutafuta ushindi na kuwapa burudani mashabiki wao kwa kuonesha kiwango cha juu namna ambavyo wamekuwa wakicheza kila mchezo.
-
Amesema licha ya kupata ushindi ugenini anaamini mechi ya nyumbani itakuwa bora zaidi kwa upande wao kwa kuwa wanacheza kwenye mazingira waliyoyazoea.
"Muhimu kuja kucheza nyumbani iwe New Amaan Complex au Azam, tupo nyumbani kazi yetu kucheza na kuhakikisha tunashinda mchezo dhidi ya CBE kwa kuendelea kupata ushindi mnono,” amesema Aziz Ki.
Mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Abebe Bikila, Septemba 14, Yanga iliondoka na ushindi wa 1-0 bao likifungwa na mshambuliaji Prince Dube.