Katika mahojiano ya hivi majuzi kwenye chaneli rasmi ya YouTube ya Echo Room, mwimbaji maarufu wa Nigeria Portable amefunguka kuhusu kukutana kwake na mwimbaji mwenzake Davido huko Amerika.
Portable pia alifichua kwanini ameamua kuacha kumuomba Davido collabo kwenye nyimbo zake.
Wakati wa mahojiano, Portable alidai kuwa yeye ni tajiri kuliko Davido na alionesha kutotaka kumsujudia.
Akisimulia tukio hilo, anasema alilazimika kughairi moja ya onesho lake, ambalo lilikuwa na thamani ya dola 6,000, ili kuweza kula chakula cha jioni na Davido baada ya mwaliko wake.
“Nilikuwa marekani nikitafuta msanii wa kigeni wa kufanya naye kolabo kabla Davido akanialika kula chakula cha jioni naye. Ilinibidi kughairi show yangu moja yenye thamani ya $6,000, ili niwe na Davido,” alisema Portable.
Kwa mujibu wa mtandao wa Portable, Davido alikuwa ameahidi kumshirikisha katika moja ya nyimbo zake lakini wakati wakiendelea kujiburudisha kwenye klabu, mwimbaji Zlatan Ibile alidaiwa kumpigia simu Davido na kumshauri asijihusishe na Portable.
Kisa cha kusisitiza jambo hilo ni kutokana na tukio lililowahi kutokea baina yao kipindi cha nyuma, na simu hiyo inaonekana imepelekea kumfanya Davido sbadili mawazo yake kuhusu kolabo.
Portable alieleza kusikitishwa kwake na kusema, “aliniahidi kuwa atanishirikisha katika moja ya nyimbo zake na tulipokuwa tukiburudika pamoja kwenye klabu moja, mwimbaji Zlatan Ibile alimpigia simu na kumwambia asiwe na uhusiano wowote nami.