MwigizajiTyrese Akamatwa na Polisi Kwa Kushindwa Kulipa Matunzo ya Mtoto Milioni 27 Kwa Mwezi

Tyrese Gibson alikamatwa mahakamani Jumatatu asubuhi kwa kushindwa kulipa matunzo ya mtoto kwa mke wake wa zamani, Samantha Lee.


Kwa mujibu wa TMZ, muigizaji huyo wa “Fast & Furious” ambaye yeye na Samantha wana mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 5 aitwaye Soraya – alifikishwa mbele ya Jaji Kevin Farmer kwenye mahakama ya Fulton County, Georgia, kwa kesi yake ya matunzo ya mtoto.


Inaripotiwa kuwa jaji alikuwa amechoshwa na Tyrese kukataa kulipa shilingi milioni 27 kwa mwezi kama alivyoamriwa kuanzia Aprili mwaka jana. Kwa sababu ya kutolipa, Jaji Farmer alimshikilia Tyrese kwa kudharau mahakama.


Aliwekwa pingu na kuondolewa mahakamani.


Kwa mujibu wa taarifa, Jaji Farmer alisema Gibson angeweza kuepuka kifungo ikiwa atailipa jumla ya shilingi milioni 200.6, ikiwa ni pamoja na shilingi milioni 20.4 za ada za wakili wa Samantha Lee.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii