DJ DAVIZO KUWANIA TUZO ZA TMA AKIWA NA PARTY LOVER

Msanii wa muziki wa miondoko ya dancehall ambaye anawakilisha jiji la Arusha David mchome maarufu kwa jina la Dj Davizo a.k.a bunduki mwaka jana alifanikiwa kuachia single kadhaa kikiwemo ting’a ling ,wedding day Pamoja na nyingine huku mwaka 2024 alianza kwa kuachia ep yake yenye ngoma saba ndani yake akiwa ameshirikiana na wasanii kama young lunya,cooly chata,country wizzy na wengine ep ambayo aliipa jina la unstopabble ambayo pia ina ngoma kadhaa zilizofanya vizuri ikiwemo gonga .

Mwaka huu kupitia tuzo za muziki Tanzania ni moja ya msanii ambaye ametajwa kuwania kipengele cha mwanamuziki bora wa muziki wa dancehall na kipingele cha wimbo bora wa muziki wa dancehall wa mwaka wimbo wake wa Ting’a ling ambao video ya wimbo huo umefanyika katika nchi tofauti tofauti.




Wakati akiwa amechaguliwa kuwania tuzo za muziki Tanzania mwaka huu pia ameachia wimbo wake mpya akiwa amemshirikisha Mwamba wa kaskazini Joh makini wimbo ambao unafahamika kwa jina la “Party lover” ikiwea sehemu ya muendelezo wake wa kuachia kazi zake za muziki.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii