Man United ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 14, katika mechi tatu za mwanzo za EPL imeshinda moja na kupoteza mbili.
Kutokana na kuanza vibaya, wachambuzi na mashabiki wengi wamekuwa wakimshambulia Ten Hag wakiamini yeye ndio tatizo kwani timu imetumia zaidi ya Pauni 200 milioni kwa ajili ya kufanya maboresho mbalimbali ikiwa pamoja na kuwasajili Joshua Zirkzee, Leny Yoro, Manuel Ugarte na Matthijs De Ligt.
Ripoti zinadai Ten Hag yupo kwenye presha kubwa ya kufutwa kazi ingawa baadhi ya viongozi wa juu wa timu hiyo bado wanataka aendelee na wana imani naye.
Kwa upande wake Shearer anaamini kocha huyo ana michezo miwili tu inayofuata kuamua juu ya hatma yake ikiwa atabakia au laa.
"Kwa matokeo ya Man United timu inahitaji kubadilika kwa haraka ili Ten Hag aendelee kuwa kibaruani kwenye hadi Krismasi, naona kubakia kwake kunategemea sana na kile kitakachofanyika katika mechi mbili zinazofuata."
"Baada ya kufungwa na Brighton na jinsi walivyopoteza kwa Liverpool, ikiwa timu haitabadilika katika mechi zijazo, itakuwa vigumu sana kwake kubakia kwa sababu kelele zitazidi kuwa kubwa."
Baada ya mapumziko ya kimataifa, Man United itasafiri hadi St Mary's kwa ajili ya kucheza na Southampton, ambao bado hawajapata hata pointi moja tangu kuanza kwa ligi hii.