Walimu Wanne Mbaroni Kwa Kuwajeruhi Wanafunzi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limetolea ufafanuzi kuhusu tukio lililotokea la mwanafuzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Mnadani ambaye anadaiwa kupewa adhabu kuchapwa viboko na walimu wanne na kusababishiwa majeraha katika mwili wake.


Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Katabazi amesema tukio hilo lilitokea Agosti 23, 2024 ambapo watuhumiwa hao ambao ni walimu wamekamatwa kwa mahojiano zaidi.


Kamanda katabazi amesema kuwa taarifa za awali zinaeleza kuwa walimu hao waliwapa adhabu hiyo wanafunzi wanne wa kike kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya mapenzi shuleni hapo, ndipo mwanafunzi mmoja akajeruhiwa vibaya kutokana na adhabu hiyo na kukimbizwa hospitali ya Serikali ambapo alilazwa lakini wenzake waliendelea vizuri.


Aidha, Kamanda katabazi amesema kuwa Jeshi linaendelea na uchunguzi iwapo adhabu iliyotolewa ni kwa mujibu wa taratibu, sheria ama kama kuna taratibu zilikukwa kabla ya kuchukua hatua zaidi za kisheria.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii