Sakata la kufungia mtandao wa TikTok lafika pabaya

Kubwa kwa sasa kwenye upande wa teknolojia ni kufungiwa kwa mtandao wa TikTok nchini Marekani, ripoti za awali zinasema ifikapo tarehe 19 mwezi huu itakuwa ngumu kwa mtumiaji wa TikTok kutokea nchini humo kupata huduma za mtandao huo.

Mtandao huo unaomilikiwa na kampuni ya ByteDance, unashambuliwa na mamlaka za juu ikiwemo mahakama, kwa kile wanachodai kuwa usalama wa taarifa za watumiaji wa mtandao huo kutokea nchini Marekani kuwa mdogo.

Kupitia ukurasa rasmi wa mtandao ''X'' wa mtengeneza maudhui maarufu mtandaoni Mr Beast ameweka wazi nia yake ya kutamani kununua mtandao huo ili usifungiwe kwa nchini Marekani.

Mtandao wa TikTok kwa sasa una zaidi ya watumiaji milioni 170 nchini Marekani, na ifikapo tarehe 19 mtumiaji wa TikTok kutokea nchini humo itamlazimu kutumia huduma ya VPN ili kuficha utambulisho wake ndipo aweze kutumia mtandao huo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii