Wanakijiji 11 wa kijiji cha Chang’ombe kilichopo kwenye kata ya Segera wilayani Handeni, leo Januari 14, 2025 wamefariki dunia na kujeruhi wengine 11 kwa kugongwa na lori lenye namba za usajili T.680 BQW lililopoteza uelekeo wakati walipojitokeza barabarani kutoa msaada kufuatia ajali ya barabarani ya gari ndogo aina ya Tata.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt. Batilda Burian lori hilo liliwagonga watu hao usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo hivyo sambamba na majeruhi.
Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya Magunga iliyopo wilayani Korogwe na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo hiyo.